What's New
Speeches
Mkereketwa
Official Policy Documents
Official Working Documents


SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM YA TAIFA



Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ina wajumbe wafuatao:-

 

        i.            Katibu Mkuu wa CCM ambaye atakuwa Mwenyekiti.

     ii.            Manaibu Katibu Mkuu wa CCM.

   iii.            Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni.

   iv.            Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.

      v.            Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo  ya  Siasa  na  Uhusiano  wa Kimataifa.

   vi.            Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.

 vii.            Makatibu   Wakuu   wa   Jumuiya   za Wananchi zinazoongozwa na CCM.

 

Majukumu  ya  Sekretarietiya Halmashauri  Kuu  ya  Taifa  ni:-

·         Kusimamia shughuli zote za utendaji za Chama kitaifa.

·         Kuandaa shughuli za vikao vya Chama ngazi ya Taifa.

 

Majukumu ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa yanagawanyika ifuatavyo:-

(a)    Katibu Mkuu wa CCM.

(b)    Idara ya Organaizesheni.

(c)     Idara ya Itikadi na Uenezi.

(d) Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

(e)    Idara ya Uchumi na Fedha.

Kila  Idara  inaongozwa  na  Katibu  wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Idara ya  Utawala  na  Uendeshaji  Bara  au Zanzibar  inaongozwa  na  Naibu  Katibu Mkuu wa CCM

 

Kila Idara ya Makao Makuu ya Chama inakuwa  na  Kamati  ya  Ushauri  yenye Wajumbe wasiozidi watano akiwemo na Katibu  wa  Halmashauri  Kuu  ya  Taifa.Wajumbe hao watateuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

   

Habari Zaidi:

   
     

ccm flag



Email
Links
Contact Us
CCM Creed   Conditions for Membership   Aim and Objectives

Chama Cha Mapinduzi believes that all human beings are equal

 

It is easy to be a member of CCM as its conditions for membership are directed towards an integrity citizen

 

CCM aims at defending the independence of our country and the freedom of its citizens

© COPYRIGHT 2002-2010
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
P.O. BOX 50, DODOMA - TANZANIA [TELEFAX: +255-22-2185245; EMAIL: katibumkuu@ccmtz.org]