|
Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa
Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa unaundwa na wajumbe wafuatao:- i. Mwenyekiti wa CCM. ii. Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na CCM. iii. Makamu wawili wa Mwenyekiti wa CCM. iv. Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM. v. Katibu Mkuu wa CCM. vi. Manaibu Katibu Mkuu wa CCM. vii. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni. viii. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi. ix. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. x. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha. xi. Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa. xii. Wabunge wote wanaotokana na CCM au kama Bunge limevunjwa wale wanachama wote waliokuwa Wabunge mara kabla ya kuvunjwa Bunge. xiii. Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wanaotokana na CCM au kama Baraza hilo limevunjwa wale wanachama wote waliokuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi mara kabla ya kuvunjwa kwa Baraza hilo. xiv. Makatibu wa Siasa na Uenezi wote wa Mikoa. xv. Makatibu wa Uchumi na Fedha wote wa Mikoa xvi. Wenyeviti wote wa CCM wa Wilaya. xvii. Makatibu wote wa CCM wa Wilaya. xviii. Makatibu wote wa Siasa na Uenezi wa Wilaya. xix. Makatibu wote wa Uchumi na Fedha wa Wilaya. xx. Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wabunge wote wa CCM. xxi. Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wanaotokana na CCM. xxii. Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti kutoka kila Jumuiya ya Wananchi inayoongozwa au iliyojishirikisha na CCM ambao ni wana-CCM. xiii. Wajumbe watano waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa kila Wilaya.
x. Mwenyekiti, Katibu wa Mkoa na Mjumbe mwingine mmoja aliyechaguliwa kutoka kila Mkoa wa Bara na Zanzibar kwa kila Jumuiya ya wananchi
|
|
Habari Zaidi: |
||




