KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Kazi za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ni:
(1) Kutoa uongozi wa Siasa katika nchi.nn
(2) Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za CCM.
(3) Kueneza Itikadi na Siasa ya CCM nchini.
(4) Kusimamia kampeni za Uchaguzi na kampeni nyinginezo.
(5) Kuteua Makatibu wa CCM wa Wilaya,Katibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, Makatibu Wasaidizi Wakuu wa Idara na Wakuu wa Vitengo vya Makao Makuu ya Chama.
(6) Unapofika wakati wa Uchaguzi Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa inashughulikia mambo yafuatayo:-
(a) Kufikiria na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya Wanachama watakaosimama katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM.
(b) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu majina ya Wanachama wasiozidiwatano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(c) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya Wanachama watakaosimama katika uchaguzi wa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM.
(d) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya Wanachama wasiozidi watatu ambao wanaomba kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar.
(e) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya Wanachama wanaoomba nafasi za uongozi katika CCM ambao uteuzi wao wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
(f) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya Wanachama wanaoomba nafasi ya Ubunge na Wanachama wanaoomba nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.
(g) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa juu ya Wanachama wa CCM wanaoomba nafasi za uongozi katika Jumuiya za Wananchi zinazoongozwa na CCM, ngazi ya Mkoa na Taifa, ambazo uteuzi wake wa mwisho hufanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
(7) Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote isipokuwa Mwenyekiti wa CCM na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uongozi.
(8) Kuona kwamba masuala ya Ulinzi na Usalama wa Taifa na Maendeleo yanazingatiwa.
(9) Kuandaa mikutano ya Halmashauri Kuu ya\CCM ya Taifa.
(10) Kuwa na mikakati endelevu ya kuimarisha Chama kimapato, kudhibiti mapato na mali za Chama na kuthibitisha matumizi ya Chama katika ngazi ya Taifa.
|
|
Habari Zaidi: |
||




